STORY MPYA

recent

BALOZI SEFUE: MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI HAYAVUNJI SHERIA YA UNUNUZI


Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema maagizo ya Rais Magufuli kutaka fedha zilizokuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima, kupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, hayavunji sheria ya manunuzi wala utaratibu mwingine wa kisheria.

Hivi karibuni,Rais Magufuli aliagiza sh.milioni 225 zilizokuwa nimechangwa kwa ajili ya hafla ya wabunge zipelekwe Hospitali ya Muhimbili kununua Vitanda na Mashuka.

Aligiza pia Bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sherehe za Uhuru Disemba 9 zitumike kupanua barabara ya Mwenge- Morocco

Akitoa ufafanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco, Balozi Sefue amesema mradi huo sio mpya na kwamba taratibu zote zilishafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa waliokuwa wamejenga kando ya barabara.

Amesema kilichokuwa kinakwamisha mradi huo ni pesa.

Akizungumzia sakata la wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyima likizo wafanyakazi huku wengine wakitiwa rumande kwa masaa 6, Balozi Sefue amesema serikali haina taarifa rasmi hivyo akalitaka shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kuwasilisha malalamiko serikalini badala ya kuishia kulalamika katika vyombo vya habari.
BALOZI SEFUE: MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI HAYAVUNJI SHERIA YA UNUNUZI Reviewed by Unknown on 11:50 AM Rating: 5
All Rights Reserved by TANZANIA COUNTRY BLOG © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.