DAR ES SALAAM: ASKARI 6 WAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI
Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba.
Mbele ya Hakimu Simba, Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kisheni, aliwataja washtakiwa kuwa ni Inspekta Bon Mbange mkazi wa Magomeni, F 919 Sajenti Filbert Nemes na Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili, Asubile Mwakyusa, Deogratius Mwageni na Joseph Jimmy.
Kisheni alidai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Desemba 19, mwaka huu maeneo ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, waliwaua Yasin Rashid na Samson Msigale.
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alieleza kukamatwa kwa washtakiwa hao wakihusishwa na utata wa mauaji ya wafanyabiashara hao.
Kamanda Kova alidai taarifa zilidai kuwa Rashid na Samson wanaodaiwa kuwa ni majangili, waliuawa wakati wakirushiana risasi na askari hao wa kikosi maalumu cha kukabiliana na ujangili maeneo ya Sinza.
Pia alidai pamoja na askari hao sita kukamatwa mwingine aitwaye Issa Kazimoto anatafutwa na polisi baada ya kukimbilia kusikojulikana.
DAR ES SALAAM: ASKARI 6 WAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI
Reviewed by Unknown
on
1:27 PM
Rating: