WATU 30 WAMEOKOLEWA BAADA YA KIVUKO CHA KILOMBERO KUPINDUKA JANA USIKU
Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi na kukifanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji jana usiku.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa leo Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama, kivuko hicho kilikuwa na watu 31, magari na mizigo mbalimbali ambapo mpaka sasa mtu mmoja bado hajapatikana.
Tukio la kivuko hicho cha mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza.
WATU 30 WAMEOKOLEWA BAADA YA KIVUKO CHA KILOMBERO KUPINDUKA JANA USIKU
Reviewed by Unknown
on
10:00 AM
Rating: